TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Katavi imewafikisha mahakamani watumishi saba wa serikali kwa tuhuma za kujihusisha na ubadhilifu wa fedha za serikali zaidi ya shilingi bilioni 1.23
Akizungumzia ubadhilifu huo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Faustine Maijo amesema kufuatia uchunguzi waliofanya kwa muda wa zaidi ya wiki mbili uliowahusisha watumishi hao, walibaini kufujwa kwa fedha na watumishi hao kutoka Halmashauri ya Mpimbwe, Manispaa ya Mpanda na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Katavi.
Amesema uchunguzi umethibitisha kuwa fedha hizo ambazo ni zaidi ya bilioni moja zililipwa kwa watu binafsi ambao hawakua na kazi zozote walizofanya katika halmashauri hiyo na walikuwa ni watu ambao wanafahamiana nao.