National News

"WANACHI HAWAKUPENDA KUCHUKUA TAHADHARI YA KUHAMA" - MATINYI

Tarehe: 12 Apr, 2024


Wananchi walipewa taarifa ya uwepo wa mafuriko ila wengi hawakupenda kuchukua hatua za kuhama kwenye hayo maeneo wakidai kuwa wameshazoea changamoto hiyo ya maji kwa miaka yote ya maisha yao.

Hayo yameelezwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam hii leo, Aprili 12, 2024.

Msemaji huyo wa Serikali ameendelea kufafanua kwamba  kinachoendelea hivi sasa ni kwamba Bwawa la Mwalimu Nyerere limeshafikia ukomo wake wa kuchukua maji hivyo maji yanayozidi yanaachiwa kuendelea na safari yake ya kwenda baharini.

Amesema kutokana na mvua za El-Nino zinazoendelea kunyesha maji ni mengi kuliko kiwango cha kawaida ambacho kwa Mto Rufiji kama ni mvua za wastani hupokea mita za ujazo 1,400 hadi 2,000 kwa sekunde lakini kwa sasa ni zaidi ya mita za ujazo 8,000 ambazo mto unapokea kwa sekunde.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab