National News

TASAC YASEMA MELI ILIYOZAMA ZIWA TANGANYIKA INATOKA DRC

Tarehe: 08 Apr, 2024


Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limesema meli iitwayo MV Maman Benita, iliyozama katika eneo la Kabimba, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) ni mali ya kampuni kutoka nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na TASAC, leo Aprili 8, 2024; imesema meli hiyo imesajiliwa chini ya bendera ya DRC na inamilikiwa na kampuni ya Kikongo, iitwayo Établissement Manimani.

Kabla ya kuzama kwa meli hiyo katika Ziwa Tanganyika, ilianza safari yake Aprili 6, 2024 saa 12:00 jioni ikitokea bandari ya Kigoma kuelekea Kalemie, DRC; ikiwa imebeba jumla ya abiria 27.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab