National News

WAETHIOPIA 17 MBARONI KWA KUINGIA NCHINI KINYEMELA

Tarehe: 08 Apr, 2024


Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara Aprili 07, 2024 wamethibitisha kuwakamata watu 17 raia wa kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila ya kufuata utaratibu ikiweno kutokuwa na vibali.

Akizungumzia tukio hilo ofisini kwake,Kaimu Kamnda wa Polisi Mkoa ea Manyara ,Kamishna Msaidizi wa Polisi-ACP Lucas Mwakatundu amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kijiji cha Kiongozi ,Kata ya Maisaka, Tarafa ya Babati ,Wilaya ya Babati wakiwa wanasafirishwa kwenye gari aina ya V8 VXR yenye namba za usajili STL 1964.

Mwakatundu amewaomba wananchi na jamii kwa ujumla kushirikiani na Polisi katika kuhakikisha hakuna magendo yanayopitishwa kwa kutoa taarifa za watuhumiwa wa uhalifu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara pia limewaonya watanzania wasio wazawa kuacha mara moja kujihusisha na usafirishaji wa magendo ikiwemo wahamiaji haramu , dawa  za kulevya na nyara za serikali.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab