National News

NDEJEMBI AKUTANA NA KUTETA NA VIONGOZI TUCTA

Tarehe: 07 Apr, 2024


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya kikao na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na kukagua maendeleo ya ukarabati wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambamo sherehe za maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu zitafanyika.

Ndejembi ameelekeza kuwa hadi kufikia Aprili 15, 2024 ukarabati wa uwanja uwe umekamilika lakini pia ameelekeza idadi ya mafundi kuongezwa ili kasi ya ujenzi iongezeke.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Maganga pamoja na viongozi wa shirikisho hilo wakiongozwa na Rais wao, Tumaini Nyamhokya.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab