National News

TMA YATABIRI UWEPO MVUA KUBWA

Tarehe: 06 Apr, 2024


Utabiri wa hali hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) uliofanyika umeonesha kuwa kuanzia leo Jumamosi, Aprili 6 hadi 9, 2024 kutakuwepo na mvua kubwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha mikoa mingine iliyotajwa ni pamoja na Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga na Kigoma.

Kutokana na hali hiyo ya mvua hizo kubwa, mamlaka hiyo imeonesha uwezekano wa kutokea athari kwa makazi kuzungukwa na maji, na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi ambapo imewataka  wananchi kuzingatia na kujiandaa kwa hali hiyo.


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab