National News

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA ZANA ZA KISASA

Tarehe: 08 Aug, 2023


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wananchi kutumia mbinu na maarifa mapya ikiwa ni pamoja na kujiimarisha katika matumizi ya teknolojia kwa lengo la kuongeza tija katika uzalishaji mali na kujiletea maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kilele cha maonesho ya Sikukuu ya wakulima Nanenane kanda ya Magharibi yaliyofanyika mkoani Tabora ambapo amesema jamii inatakiwa kutumia zana za kisasa kuendesha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwemo matumizi ya mashine pamoja na kujiongezea maarifa ya kiutendaji.

Maonesho ya Sikukuu hizo ambayo kitaifa yamefanyikia Mbeya yameongozwa na kaulimbiu isemayo "Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo endelevu ya Chakula"

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab