National News

SERIKALI IMETENGA BIL.1.7 POSHO WENYEVITI SERIKALI ZA VIJIJI

Tarehe: 05 Apr, 2024


Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt Festo Dugange amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetenga Sh Bilioni 1.7 hadi kufikia Februari 2024 kiasi cha Sh Bilioni 1.15 kimekwishatolewa kwa ajili ya kulipa posho za Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mtaa.

Ametoa kauli hiyo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Mhe Flatei Massay aliyehoji ni liji Serikali itawalipa posho Wenyeviti wa Vitongojo, Vijiji na kuongeza posho za madiwani ili kuwasaidia kutekeleza majukumu kikamilifu.

Amesema Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi ambapo imeendelea kulipa posho za viongozi hao ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.