UKIVAA JEZI YA AHLY, MAMELOD GETINI UTAONESHA PASPOTI
Tarehe: 19 Mar, 2024
Kuelekea michezo ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika waziri wa utamaduni, sanaa na michezo Mh. Damas Ndumbaro amewasisitiza watanzania kuwa wazalendo katika kuzisapoti timu za Simba na Yanga katika michezo hiyo.
Waziri Ndumbaro amesema atasikitishwa endapo ataona watanzania wamevaa jezi za Al Ahly katika mechi ya Simba au jezi ya Mamelod Sundowns katika mchezo wa Yanga huku akisema watu hao hawatoruhusiwa kuingia uwanjani, au wataingia kwa kuonesha Passport zinazoonesha sio Raia wa Tanzania.
“Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo ukifanya fujo Polisi watakuchukua ukapumzike kidogo utatoka baada ya mechi” - Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.