FAIDA YA AL HILAL KUSHIRIKI LIGI KUU TANZANIA BARA YAWEKWA
Tarehe: 19 Mar, 2024
“Kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) kilikaa kikachakata kwa mapana yake na kuona faida za Al Hilal kushiriki Ligi yetu na kisha kuona inafaa kuwakubalia, lakini wanashiriki kwa namna gani hilo likawa ni jambo lingine tena".
“Kwenye namna ya ushiriki wao ni kwamba watakuwepo kwenye ratiba itakapotolewa itaonekana anacheza lini na anacheza na nani lakini matokeo yatakayopatikana hayatajumuishwa kwenye matokeo ya Ligi Kuu ya NBC,” Mario Ndimbo, Afisa Habari(TFF)