National News

JENGO LA WAGONJWA WA DHARURA LATAKIWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

Tarehe: 11 Mar, 2024


Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe @ortamisemitz Dkt. Rashid Mfaume ameielekeza timu ya usimamizi wa shughuli za Huduma za Afya (CHMT) Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kusimamia kwa karibu ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) kuhakikisha linakamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo mwisho wa mwezi machi 2024.

Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo baada ya kufanya ukaguzi wa majengo pamoja na ufanisi wa utoaji huduma katika Hospitali hiyo  akiwa ameambatana na timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka ofisi ya Rais- TAMISEMI ambapo amesema majengo mengo ya wagonjwa wa dharura yamekamilika na yameanza kutoa huduma hivyo jengo hilo linatakiwa kukamila ili lianze huduma

“Tumeona vifaa vyote vipo na vimehifadhiwa kwenye jengo la maabara sasa tukamilishe kwa wakati ilil mwezi huu tuona likifanyakazi na DMO na RMO mipige picha kabisa na zirushwe tuine jengo hilo likiwa limeanza kufanyakazi na katika hospitali tulizopita katika majengo yote jemgo ambalo halijachelewa kuanza kutoa huduma ni jengo la EMD ni hapa tu halmashauri ya Uvinza” amesema Dkt. Rashid mfaume

Akisisitiza maelekezo ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange aliyatoa mwezi Januari 2024 kuhusu ukamilishwaji wa majengo katika maeneo ya kutolea huduma ifikapo April 2024 amesema maelekezo hayo yafanyiwekazi katika maeneo yote nchini na huduma zianze kutolewa.

Ikumbukwe mwezi Septemba 2023 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliagiza taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha katika ujenzi wa majengo katika Halmashauri hiyo ikiwemo lengo la EMD Uvinza huku baadhi ya wataalamu ikiwemo mkurugenzi wa Halmashauri walisimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Timu ya Afya Ustawi wa jamii na Lishe ikiongozwa na Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ipo mkoani Kigoma ikiendelea na ziara ua usimamizi shrikishi katika maeneo ya kutolea huduma za Afya ya msingi pamoja na kufuati;ia ufanisi wa huduma za Afya,Ustawi wa jamii na Lishe katika Halmashauri za mkoa wa Kigoma.