National News

WAZIRI MKUU AWAONGOZA WABUNGE KUPOKEA MAPENDEKEZO YA BAJETI

Tarehe: 11 Mar, 2024


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza Mkutano wa Wabunge wote wa kupokea Mapendekezo ya Serikali ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025.Mkutano huo umefanyika leo tarehe 11 Machi, 2024 katika ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.

Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2024/25 yaliwasilishwa na Waziri wa Ofisi ya Rais-Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo huku Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025 yakiwasilishwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.

Mara ya baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo hayo, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu kwa niaba ya Mhe. Spika alielekeza Kamati ya Kudumu ya Bajeti kuyafanyia kazi Mapendekezo hayo na kuzishauri Kamati za kisekta ipasavyo.

Kwa upande mwingine Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge takribani 14 wataanza kufanya ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo nchi nzima.

 

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab