National News

MPANGO AITAKA TBA KUFANYA UWEKEZAJI WENYE TIJA

Tarehe: 05 Aug, 2023


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango ameitaka TBA kufanya uwekezaji wenye tija katika maeneo yake na kuhakikisha wapangaji wa majengo yake wanalipa kodi kwa wakati.
 
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililo sekei jijini Arusha Dkt. Mpango ameitaka Wizara hiyo kuhakikisha inaweka msukumo kwenye ujenzi wa viwanda vya vifaa vya ujenzi ili kupunguza gharama za ujenzi hivyo kuwezesha Serikali kufikia lengo la ujenzi wa nyumba nyingi zitakazokidhi mahitaji ya ongezeko la idadi ya watu.
 
“Serikali imedhamiria kukuza sekta ya nyumba ili ichangie pato la Taifa na hivyo kukuza uchumi"amesisitiza Dkt. Mpango.

Naye Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, ameipongeza TBA kwa kujenga majengo marefu yanayohudumia idadi kubwa ya watu na kusisitiza kuwa majengo hayo yaendane na uwepo na maegesho ya magari. 
 
Aidha Mabula amesisitiza kuwa mahitaji ya nyumba nchini ni zaidi ya 390,981 kwa mwaka wakati nyumba zinazojengwa na taasisi mbalimbali kwa mwaka ni chini ya 2,000.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab