National News

RAIS MWINYI AFARIKI DUNIA

Tarehe: 29 Feb, 2024


Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Februry 29,2024 saa 11:30 jioni Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu.

Kifo hicho kimetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amesema Mzee Mwinyi ambaye alikuwa Rais kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, amekuwa akipatiwa matibabu tangu November 2023 London Uingereza na baadaye kurejea Nchini na kuendelea na matibabu Jijini Dar es sala ambapo anatarajiwa kizikwa Unguja visiwani Zanzibar Machi 2, 2024.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab