National News

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI OFISI MKUU WA WILAYA BUTIAMA

Tarehe: 27 Feb, 2024


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Butiama ambao Utekelezaji wake umefikia asilimia 60.

Mheshimiwa Majaliwa amemtaka mkandarasi wa mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo (TBA) kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa wakati.

Mpaka sasa mkandarasi ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni 843.4 ikiwa ni malipo ya awali na hati za malipo ya pili na tatu.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab