National News

IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI ARUSHA YAFIKIA 25

Tarehe: 25 Feb, 2024


Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya barabarani iliyotokea Februari 24, 2024 maeneo ya Ngaramtoni Kibaoni, Arusha imefikia watu 25 na majeruhi 21.
Ajali hiyo ilihusisha lori na magari matatu ambapo katika waliofariki, wanaume ni 14, wanawake 10 na mtoto mmoja.

Kamishina wa Polisi, Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema kati ya waliofariki, watu saba ni raia wa kigeni waliokuwa wakijitolea kufundisha katika Shule ya New Vision waliokuwa kwenye basi la shule.

Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo, pamoja na Hospitali ya Arusha Lutherani Medical Center Selian.
..................

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab