National News

15 WAFARIKI KWA AJALI YA LORI NA MAGARI MADOGO MATATU

Tarehe: 25 Feb, 2024


Watu kumi na tano  (15) wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha Lori na Magari madogo matatu iliyotokea katika eneo la Ngaramtoni, mkoani Arusha ambapo inasemekana kuwa  Lori hilo  lilifeli breki, kisha kugonga magari mengine matatu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  Februari 24,2024 majira ya saa 11 jioni na kuwa ajali hiyo pia imesababisha majeruhi kadhaa ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na Selian mkoani Arusha. 


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab