National News

USAMBAZAJI UMEME UENDANE NA MAHITAJI

Tarehe: 23 Feb, 2024


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Biteko amewataka wakandarasi wa miradi ya usambazaji umeme vijijini kutekeleza kazi kwa wakati ili kuendana na kasi ya maendeleo huku akiiagiza REA kuwachukulia hatua wakandarasi wazembe.

Ameyasema hayo baada ya kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Mkangwe wilayani Mufindi ambapo amesema usambazaji umeme vijijini mkoani Iringa umefanyika kwa asilimia 100 ambapo vijiji vyote 360 mkoani humo vimesambaziwa umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Aidha, amewapongeza Wakandarasi wa umeme vijijini waliofanya  kazi ya usambazaji mkoani Iringa ambayo imepelekea vijiji vyote mkoani humo kuwa na umeme kufikia Desemba 2023.

Akiwa katika Kijiji cha Mkangwe, Dkt. Biteko alizindua  Zahanati ya Kijiji cha Mkangwe ambapo aliagiza uongozi wa Halmashauri wilayani Mufindi kuhakikisha Zahanati hiyo inaanza kuhudumia wananchi ipasavyo kufikia jumatatu ya tarehe 26 Februari 2024 baada ya huduma ya umeme kufika kwenye zahanati hiyo na hii ikijumuisha kuwepo kwa Rasilimali Watu na Vitu.
..........................
Powered by 
@tigo_tanzania
#TigoTanzania
#TigoMainfm

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab