International News

SERIKALI KUBORESHA RELI YA TAZARA

Tarehe: 16 Feb, 2024


Naibu waziri Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amelieleza Bunge mpango wa Serikali kuanza uboreshaji wa Reli ya TAZARA yenye urefu wa Kilometa 1860 kutoka Dar es Salaam hadi Kapili Mposhi, Zambia.

Naibu Waziri Kihenzile ameeleza hayo leo Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema kuwa sasa kinachoendelea ni mazungumzo kati ya Serikali za Tanzania, China na Zambia ili baada ya uboreshaji reli hiyo iweze kujiendesha kibishara.

Naibu Waziri David Mwakiposa wakiposa Kihenzile pia ametumia Ukurasa wake wa Instagram kueleza kuhusu jambo hilo ambapo amesema - "Reli hii yenye urefu wa Kilometa 1860 ambapo Tanzania ni Kilometa 975(52%) na Zambia ni km 885(48%) iliyoanza kufanya kazi tatehe 14.07.1976 kwa sheria Na 23 ya mwaka 1975, Reli  ikiwa na Madaraja 319, Mahandaki 22 na makalavati 2269 yenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani milion tano."