National News

WAGANGA WAFAWIDHI KUPEWA POSHO

Tarehe: 15 Feb, 2024


Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema kuanzia mwaka wa fedha ujao waganga wafawidhi katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi wataanza kupewa posho ya madaraka kwa kazi kubwa wanayofanya kwenye ngazi ya msingi.

Akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi Februari 14, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema waganga wafawidhi wanastahili kulipwa posho hiyo na ameahidi kuanzia July,2024 itaanza kutolewa kwa wataalam hao muhimu.

"Wanganga Wafawidhi mnafanya kazi kubwa kwenye vituo vya kutolea huduma ninyi ndio madaktari, wafamasia, wataalam wa maabara, mnasimamia ujenzi wa miradi ya serikali hakika mnastahili kulipwa posho hii naenda kuonana na wadau na katika fedha tutakazopewa kiasi kitatumika kwa ajili ya kulipa posho hii" amesisitiza Ummy. 

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab