National News

VIBANDA ZAIDI YA 100 VYATEKETEA KWA MOTO KIGOMA

Tarehe: 10 Feb, 2024


Vibanda zaidi ya 100 vimeteketezwa na moto uliozuka majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo Februari 10, 2024 katika soko la mitumba (Selemala) lililopo Mwanga Manispaa ya Kigoma - Ujiji.

Kaimu Kamanda wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kigoma, Jacob Chacha amesema  mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine likiwemo Jeshi la Polisi walifanikiwa kuzima moto huo na hivyo kuwezesha vibanda vingine zaidi ya 600 kusalimika.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo na kwamba pamoja na vibanda hivyo kuteketea kwa moto hakuna mtu aliyejeruhiwa ama kufariki dunia.

Moto huo umeteketeza zaidi ya vibanda 100 katika Soko hilo linalotajwa kuwa na zaidi ya vibanda vya wafanyabiashara zaidi ya 780.
..........................
Powered by 
@tigo_tanzania
#TigoTanzania
#ValentinesLoversNight
#TigoMainfm

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab