Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ameonesha kuchukizwa na tabia za Wakurugenzi wengi nchini kutolipa madeni ya watu wanaowadai yakiwemo malimbikizi ya watumishi wa waliostaafu na baadhi ya kampuni walizozipa tenda katika miradi mbalimbali.
Hilo limejibainisha zaidi mara baada ya Mwenezi Makonda kukutana na Malalamiko ya wananchi wengi wakidai pesa zao kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi wakati akizungumza na Wananchi akiwa mkoani Rukwa.
Katika malalamiko hayo, Mwanamama aliyejitambulisha kwa jina la Catherine amelalamika kudai pesa zake Tsh Milioni 4.04 baada ya kustaafu tangu Septemba, 2020 na tayari ana waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi ukimthibitisha kutakiwa kulipwa madai yake tangu mwaka 2020 na bado hajalipwa.