National News

MAKONDA ATUA KIGOMA KWA ZIARA

Tarehe: 02 Feb, 2024


Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Makonda amewasili wilayani Kakonko mkoani Kigoma, kuendelea na ziara yake ya mikoa 20 ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM kwa mwaka 2020/25.

Akihutubia wananchi wa Kakonko, Makonda ameonesha kufahamu kuhusu changamoto kadhaa zilizopo wilayani Kakonko na kuahidi kuendelea kuisukuma serikali katika kupata ufumbuzi wake.

Wakati wa ukaribisho wake mkoani Kigoma Mwenezi Makonda pia ameendeleza utamaduni wake wa kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa papo kwa papo kutoka kwa wahusika.

Mwenezi Makonda pia ametawazwa kuwa Mwami wa wilaya ya Kakonko ikiwa ni utamaduni wa watu wa Kigoma,  pamoja na kukabidhiwa vazi maalum na silaha za jadi kama kielelezo cha kumpa ujasiri kwenye majukumu yake.
..........................
Powered by 
@tigo_tanzania
 #TigoTanzania #ValentinesLoversNight #TigoMainfm

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab