National News

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA MIKOA NANE

Tarehe: 29 Jan, 2024


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo juu ya uwepo wa vipindi vifupi vya mvua kubwa  katika mikoa nane Tanzania bara. 

Mikoa hiyo ambayo itakumbwa na hali mbaya ya hewa ikiwemo mvua kubwa ni Morogoro, Iringa, Lindi, Mbeya, Mtwara, Njombe, Songwe na Ruvuma.

Utabiri huo wa TMA umetolewa leo Januari 29, 2024 na kufafanua kuwa upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya Km 20 kwa saa kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini na kwa kasi ya Km 30 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini. 

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.

Imeeleza kwa siku ya Jumatano Januari 31, 2024 kuendelea kwa mvua katika baadhi ya maeneo.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab