National News

KIGOMA YAPIGA HATUA KUKABILIANA NA UDUMAVU

Tarehe: 04 Aug, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Thobias Adengenye amewataka Wakuu wa Wilaya kusimamia vikao vya kila robo vya tathimini ya lishe ili kuweza kuendelea kuondoa hali ya udumavu kwa Watoto 

Andengenye ameyasema hayo katika kikao cha tathimini ya lishe kwa Mkoa kilichofanyika na kikihusisha Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu, Maafisa lishe, Wakuu wa Mipango, na Wakuu wa idara ya Fedha kutoka Sekritarieti ya Mkoa na Halmashauri

Aidha amesema kuwa  kwa kipindi cha Miaka mitatu Mkoa wa Kigoma umepunguza hali ya udumavu kutoka  asilimia 42 hadi  asilimia 27 kwa hali ilivyo kwa sasa na kuongeza katika kuondoa udumavu lazima elimu iendelee kutolewa kuanzia ngazi ya familia wakiwemo Wanaume jambo litakalosabisha ukuaji wa uzalishaji Mali pamoja na kukua kwa uchumi katika Mkoa wa Kigoma

Naye Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu. Albert Msovera amewataka Maafisa lishe kukagua chumvi zinazouzwa katika minada kama zinakidhi viwango na kuwa na madini Joto kwa afya ya walaji

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab