National News

MWENYEKITI UVCCM TAIFA ARIDHISHWA NA USIMAMIZI MIRADI

Tarehe: 27 Jan, 2024


Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Mohamedi Ali Kawaida  Januari 26, 2024 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na kuoneshwa kuridhishwa na usimamizi wa miradi hiyo.

Ziara hiyo ameifanya mara baada ya kuwasili Mkoani Kigoma January 24, 2024 kwa ziara ya Kikazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Katika ziara kiongozi huyo amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja kwa namna anavyosimmia miradi ya maendeleo

Miradi aliyotembelea ni pamoja Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa unaoendelea Kata ya Kagera, Shule mpya inayojengwa eneo la Mji mwema Kata ya Kigoma, Mradi wa Vijana wanaotengeneza Mikate( Wanufaika 10%) na kutembelea Chanzo kinachozalisha Maji (Aman beach) kinachosimiwa na KIUWASA
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab