National News

TAWI CHUO KIKUU MUHAS KUJENGWA KIGOMA

Tarehe: 25 Jan, 2024


Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu  cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye Ofisini kwake Leo Januari 25, 2024.

Akiwa Mkoani hapa, Prof. Kamuhabwa ametembelea na kukagua eneo linatotarajiwa kuanza kufanyika kwa ujenzi wa Tawi la Chuo hicho Mkoa wa Kigoma pamoja na kupokea taarifa za hatua mbalimbali za maandalizi ya ujenzi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kupitia mazungumzo hayo, Mkuu huyo wa Mkoa ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuelekeza mradi huo mkubwa mkoni hapa kwani utasogeza huduma za  kibingwa na bobezi kimatibabu, kuongeza ikama ya watoa huduma ya Afya pamoja na  kuongeza fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wakazi.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab