International News

RAIS WA LIBERIA ASHINDWA KUMALIZIA HOTUBA

Tarehe: 23 Jan, 2024


#Habari: Rais mpya wa Liberia, Joseph Boakai (79) ameshindwa mara mbili kumalizia hotuba yake Januari 22, 2024 wakati wa sherehe za kuapishwa kwake na kulazimika kuondolewa jukwaani kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni uchovu uliosababishwa na joto kali. 

Boakai ndiye Rais mzee zaidi kuwahi kuhudumu nafasi hiyo nchini Liberia ambapo alimshinda Rais George Weah aliyekuwa anawania muhula wa pili.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab