Sports

MWANGA CITY QUEENS YANG'ARA LIGI YA MIKOA

Tarehe: 25 Jul, 2023


Mwanga City Queens imetinga fainali ya ligi ya mabingwa wa mikoa baada ya kuitandika Sayari Woman ya Dar es salaam mabao 2-1. Mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nyamagana Mkoani Mwanza.

Mabao ya Mwanga City Queens  yamefungwa  na Christina Chimpaye dakika ya 33 na Christa Bella dakika ya 47 huku goli la kufutia machozi la Sayari Woman likifungwa Dak ya 30 na Magreth Mwakyamba.

Mwanga City Queens atakutana na GETS PROGRAM ya Dodoma kwenye mchezo wa fainali.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab