National News

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI MKUU WA CHINA

Tarehe: 23 Jan, 2024


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumanne Januari 23, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye aliwasili nchini jana Jumatatu Januari 22, 2024 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Mazungumzo ya viongozi hao wawili yamefanyika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam kuhudhuriwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko na viongozi wa Serikali kutoka Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania.

Waziri Mkuu ujio wa kiongozi huyo unatokana na mahusiano mazuri yaliyopo tangu enzi za Waasisi wa nchi hizo mbili ambapo mahusiano hayo yameendelea kunufaisha wananchi wa Tanzania na China, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.

“Mazungumzo yetu leo yamegusa masuala ya kiuchumi tukizingatia propramu ya sasa ya nchi ya Tanzania ya kukuza uchumi, pia tumezungumzia masuala ya biashara na uwekezaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile viwanja vya ndege, barabara na uboreshaji wa nishati ya umeme.”

Kuhusu uwekezaji amesema kuwa, China inafanya uwekezaji hapa nchini ikiwemo kwenye ujenzi wa miundombinu akitolea mfano ujenzi wa reli ya kati ambao sasa unaendelea na China imetoa mkopo wa gharama nafuu, pia imewekeza kwenye mradi wa Makaa ya Mawe Liganga na Mchuchuma na Viwanda.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa, viongozi hao wamezungumza kuhusu uimarishaji wa mipango mikakati ya nchi ya China kwa nchi za Afrika (FOCAC) ambapo FOCAC imedhamiria kusimamia maendeleo ya Afrika katika afya, elimu, miundombinu na nishati na kwamba Tanzania tayari imewasilisha miradi nane.
@owm_tz
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania





  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab