National News

MWENYEKITI UVCCM TAIFA AWASILI KIGOMA

Tarehe: 22 Jan, 2024


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye Leo Januari 22, 2024 amempokea Mwenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa, Mohammed Kawaida anayetarajia kuanza Ziara ya kikazi Mkoani hapa.

Akizungumza mara baada ya kupokelewa na Mamia ya wanachama wa Chama hicho, kiongozi huyo amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuendelea kuimarisha hali ya usalama na amani mkoani hapa, jambo linalotoa fursa kwa wakazi kuwa huru katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha Kawaida amewakumbusha wanachama wa CCM mkoani Kigoma kuendelea kuyatangaza mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab