National News

WALIMU WATAKIWA KUZINGATIA RATIBA ZAO SHULENI

Tarehe: 18 Jan, 2024


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja Leo Januari 18, 2024 ameendelea kufanya ziara kwa Shule za Msingi zilizopo  katika Manispaa hiyo kwa lengo la kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji.

Katika ziara hiyo Mkurugenzi huyo amewataka Walimu kuendelea kusimamia ufundishaji kwa kuzingatia ratiba ya vipindi kwa kila juma, Wiki na Mwezi ili kukuza viwango vya ufaulu .

Aidha amewataka kuendelea kusimamia maadili ya Wanafunzi na kuwalinda dhidi ya Vitendo vya ukatili vinavyoweza kutokea shuleni na katika makazi yao.  

Mkurugenzi huyo  amefanya ziara na kufanya vikao na Walimu katika Shule ya Msingi Gungu,  na Kikungu zilizopo Kata ya Gungu na Shule ya Msingi Bushabani iliyopo Kata ya Kibirizi. 


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab