National News

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS UGANDA

Tarehe: 18 Jan, 2024


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 18, 2024 ameelekea nchini Uganda ambapo anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) ulioanza Januari 15 - 20, 2024.

Pia Mheshimiwa Majaliwa atahudhuria Mkutano wa Tatu wa Kusini wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+China utakaofanyika tarehe 21-22 Januari, 2024, Kampala - Uganda.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab