National News

DED KIGOMA/UJIJI AFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA ELIMU

Tarehe: 17 Jan, 2024


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja Leo Januari 17, 2024 amefanya ziara kwa Shule za Msingi zilizopo  katika Manispaa hiyo kwa lengo la kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji.

Mkurugenzi huyo amefanya ziara katika Shule ya Msingi Kibirizi, Kiheba,Buronge, Kahabwa na Rasini  ambapo amefanya vikao na Walimu huku akiwataka Walimu kufanya Ufundishaji kwa kuzingatia Kanuni na maadili ya kazi ili kuinua viwango vya Ufaulu.

Amewataka Walimu kila mmoja kujitathimini katika zoezi la Ufundishaji kwa kuhakikisha anakuwa na Maazimio ya Ufundishaji,  Maandalio ya somo, Nukuu za masomo, na uandaaji wa zana za ufundishaji.

Mara baada ya Shule kufunguliwa Mwezi Januari 2024, Mkurugenzi huyo anaendelea kufanya ziara na Vikao na Walimu kwa Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab