Sports

MKURUGENZI APIGA MARUFUKU UJENZI HOLELA KIGOMA/UJIJI

Tarehe: 25 Jul, 2023Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi.Mwantum Mgonja  amewata Wananchi na Wakazi wa Manispaa hiyo   kuepuka ujenzi holela bila kufuata taratibu za Mamlaka ya Upangaji Mji

Ameyasema Leo July 25, 2023 alipofanya ziara katika Kata na Mitaa kukagua na kudhibiti ujenzi holela bila kuwa na kibali cha ujenzi huku akisema ujenzi holela unaleta athari hasi katika upangaji wa Mji ikiwemo uvunjaji wa miundombinu mbalimbali

Aidha amewataka Wananchi kufuata taratibu za kupata kibali cha ujenzi kwa kufika katika ofisi ya Mkurugenzi idara ya Mipangomiji, na Ujenzi


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab