National News

KENYA NA TANZANIA SASA MAMBO SAFI

Tarehe: 16 Jan, 2024


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imerejesha huduma baada ya kurudisha tena vibali vya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) vya kuendesha safari za ndege za abiria kati ya Nairobi na Dar es salaam chini ya vifungu vya Haki za Uhuru wa Trafiki namba tatu na nne baada ya kutengua uamuzi wake wa jana wa kulifungia shirika hilo. 

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema wametoa ruhusa hiyo baada ya uamuzi wa Mamlaka ya Anga ya Kenya kukubali ombi la Tanzania la nchi hiyo kusafirisha mizigo yao yote kwa kutumia Kampuni ya Air Tanzania kuanzia leo January 16,2024 kwa kuzingatia Haki za Trafiki nambari tano kati ya Nairobi na Nchi za dunia ya tatu.

Hatua hiyo imekuja baada ya hapo  TCAA kutangaza zuio la KQ kutua Tanzania, saa chache baadaye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba alinukuliwa akisema amefanya mazungumzo na Waziri mwenzake anayeshughulikia masuala ya kigeni Nchini Kenya, Musalia Mudavadi ambapo wamekubaliana kumaliza sakata hilo ndani ya siku tatu . 
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania