Watu 22 wamefariki kwa kupondwa na kifusi wakati wakichimba madini ya dhahabu katika machimbo ya Ikinabushu wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Taarifa ya Kaimu kamanda wa jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu kuhusiana na tukio hilo inspector Faustine Mtitu aliyoitoa leo Januari 14, 2023 imeeleza kuwa miili 22 imeomepolewa.
"Miili yote iliyoopolewa ni ya wanaume na tayari tumemaliza kujiridhisha kuwa hakuna mwili ambao umekwama ardhini na sababu ya tukio hili ni uchimbaji holela bila kuzingatia vigezo vya usalama kwenye uchimbaji wa madini," amesema Mtitu.
Akizungumza baada ya kufika eneo la tukio waziri wa madini Anthony Mavunde ametoa utaratibu wa kuendeleza machimbo hayo ambapo amesema timu ya wizara ya madini kuwaongoza katika uchimbaji ili wachimbaji wadogo wafanye uchimbaji ulio salama.
"Kwasasa siwezi kuruhusu uchimbaji uendelee mpaka timu yangu ikae na iweke mazingira sawa ya usalama, hivyo afisi ya mkoa ifanye utaratibu wa kutengeneza kikundi ili wizara iweze kuwapatia leseni," amesema Mavunde.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania