National News

ZAHANATI YA KATA MWANGA KUSINI KIGOMA KUJENGWA HIVI KARIBUNI

Tarehe: 11 Jan, 2024


Diwani wa kata ya Mwanga Kusini Mussa Maulid amesema kuwa Halmashauri ya manispaa kigoma Ujiji Mkoani Kigoma imeshaingiza kiasi fedha kwenye akaunti ya Kata hiyo kwaajili ya ujenzi wa Zahanati ya kata ili kuwarahisishia wananchi katika eneo hilo kupata huduma ya magonjwa madogo madogo ambayo hayahitaji kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa serikali ya mtaa wa Kilimahewa na wananchi wa mtaa huo na kusema kuwa mchakato wa zabuni kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo umeshaanza na hivi karibuni Ujenzi utaanza.

"Nataka niwahakikishie kwamba hivi karibuni tumeanza michakato ya zabuni kuhusiana na suala la ujenzi wakati wowote tutaanza mchakato wa ujenzi wa zahanati yetu hiyo ya Mwanga Kusini" Alisema Maulid

Awali akizungumza kuhusiana na suala la usalama na ulinzi katika eneo la Kilimahewa Polisi kata Mwanga Kusini Rashidi Hussein amesema kuwa suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mwananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi ambapo kazi ya jeshi hilo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ulinzi na usalama huku akiwaomba wananchi kuwa na tabia ya kushiriki mikutano hiyo kwa lengo la kuweka mikakati mbalimbali ya mtaa kwa ujumla.

"Tunakuja kwenye kata ili kuja kuelimisha na kushirikiana na wananchi, ili kutatua kero za ulinzi na usalama ndiyo jukumu lililotuleta kwa kushirikiana na wananchi, na ndiyo maana mtendaji amesema umuhimu wa kukutana na wananchi ili tuelekezane na tuweke mikakati gani ya ulinzi na usalama, kwahiyo kupitia mkutano huu niwaombe tunapoitwa kwenye vikao au mikutano ni muhimu mkajitokeza kwasababu nyinyi mnajua kero lakini pia nyinyi ndiyo watu ambao tunatakiwa tushirikiane kutatua kero hizo" Alisema afande Hussein 

Sambamba na hayo pia amebainisha mikakati ya ulinzi katika eneo hilo kuwa ni pamoja na wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi hilo kwasababu wao ndiyo wanawajua zaidi wahalifu katika maeneo yao kuliko hata jeshi la polisi.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab