National News

WATUMISHI WATAKIWA KUTEMBELEA MIRADI WASIKAE OFISINI

Tarehe: 10 Jan, 2024


"TUSIFANYIE KAZI OFISINI TU" DC KIGOMA


Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kalli amewataka Watumishi wa Umma kusimamia miradi kwa ukaribu kwa kuhakisha wanakagua na kutembelea Wananchi na miradi  na kutokufanyia kazi wakiwa ofisini tu.  

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia Watumishi Leo Januari 10, 2024 katika Kikao kilichofanyikia Kigoma Social Hall kikihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa taasisi, Idara, na Vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata, Na Wakuu wa Shule. 

Amewataka Watumishi wa Umma kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu kukamilika kwa  miradi ya Maendeleo viporo  na inayoendelea kutekelezwa Wilayani hapo kwa fedha za Serikali Kuu na Mapato ya ndani.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Mganwa Nzota amewataka Watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni, taratibu na Sheria  huku akiwaagiza Wakuu wa Taasisi kuendelea kuwajengea uwezo Watumishi wanaowasimamia.


  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab