UANDIKISHAJI WANAFUNZI UENDANE NA UFAULU WA MASOMO- RC KIGOMA
Tarehe: 09 Jan, 2024
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka Walimu, Wazazi na Wanafunzi kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha uandikishaji wa Wanafunzi kwa Shule za Msingi na Sekondari unaendana na ufaulu wa Matokeo ya Mitihani.
Ameyasema hayo Leo Januari 08, 2024 alipofanya ziara Manispaa ya Kigoma/Ujiji na kukagua kuwasili kwa mara Wanafunzi wa darasa la Kwanza na kidato cha kwanza katika Shule ya Msingi Kabingo na Shule ya Sekondari Katubuka.
Mkuu huyo wa Mkoa ameridhishwa na uandikishaji na mapokezi ya Wanafunzi yanaendelea kufanyika Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku akiwataka Walimu, Wazazi na Wanafunzi kushirikiana katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua na kukuza ufaulu wa kitaaluma.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha miundombinu ya elimu ikiwemo Ujenzi wa vyumba vya Madarasa na nyumba za Walimu kwa lengo la kukuza na kuboresha Viwango vya elimu Nchini.
Mkuu huyo wa Mkoa amefanya ziara akiwa na Wenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kalli, Mbunge wa Kigoma Mjini wa Mhe.Shabani Ng'enda Kilumbe Na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja.