WAKUU WA IDARA MANISPAA KIGOMA UJIJI WATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA TACTICS
Tarehe: 05 Jan, 2024
Wakuu wa idara na Vitengo Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Awamu ya kwanza inayoanza kutekelezwa kupitia mradi wa uboreshaji wa miji kiushindani Nchini Tanzania (TACTICS).
Ziara hiyo imefanyika Leo January 04, 2024 ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Mwantum Mgonja ambapo amemtaka Mkandarasi Mjenzi kuharakisha na kukamilisha Ujenzi wa Kambi kwa wakati mwishoni mwa mwezi huu Januari ili kuendelea na ujenzi wa miradi.
Miradi hii ya Awamu ya kwanza inatekekelezwa kwa thamani ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billion ishirini na tisa ( Tsh 29,813,388,456.50/=) kwa mda wa Miezi kumi na tano.
Miradi iliyotembelea ni pamoja na Ujenzi wa kambi wa Mkandarasi unaoendelea eneo la Uwanja wa Ndege, Ujenzi wa Barabara ya Wafipa-Kagera yenye urefu wa Km 2.434, Daraja la Mto Ruiche, Ujenzi wa barabara ya Bangwe-Burega- Ujiji yenye urefu wa Km 7.1, na Ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika maeneo ya Bangwe Km 0.687, Burega Km 1.040, Rutale Km 1.263, Mlole Km 0.468 , Bushabani Km 0.581 , Mji mwema Km 0.888, na mfereji wa maji Katonyanga yenye urefu Km 0.483.