International News

MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS AACHIWA HURU KWA MSAMAHA

Tarehe: 05 Jan, 2024


Aliyekuwa mwanariadha wa Olimpiki mwenye ulemavu, Oscar Pistorius ameachiwa huru kwa msamaha nchini Afrika Kusini baada ya kukaa gerezani kwa takribani miaka 11 kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi kadhaa kupitia mlango wa bafuni mwaka 2013 na kudai kuwa alidhani ni mwizi.

Hadi hivi sasa Pistorius, ana umri wa miaka 37, alipatikana na hatia ya mauaji mwaka 2015 baada ya mahakama ya rufaa kubatilisha hukumu ya mwanzo ya mauaji bila kukusudia ingawa hata akiachiwa huru, bado ataishi chini ya masharti magumu mpaka kifungo chake kitakapomalizika mwaka 2029.

Hata hivyo kwa sheria za Afrika Kusini, wahalifu wote wana haki ya kuachiwa huru kwa msamaha mara tu watakapokuwa wametumikia nusu ya kifungo na Pistorius ameingia gerezani Oktoba 2014, alipohukumiwa kwa mara ya kwanza ambapo alikuwa mwenye mafanikio katika michezo ya Olimpiki ya Walemavu, kutokana na kushinda medali nyingi za dhahabu, na aliimarisha sifa yake baada ya kushindana na wanariadha wasio na ulemavu kwenye Michezo ya Olimpiki ya London 2012.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab