Sports

UZOEFU KWENYE TIMU YENU MNAUPATA KUTOKA WAPI?

Tarehe: 04 Jan, 2024


Rais wa Klabu ya Young Africans SC na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris Nchini Ufaransa, jana Januari 3, 2023.

Eng Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.

Licha ya mkutano huo Rais wa Yanga, Eng. Hersi alishuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa magoli 2-0.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab