Sports

AZAM USO KWA USO NA BAHIR DAR

Tarehe: 25 Jul, 2023


Timu ya soka ya Azam imepangwa kucheza na   kucheza dhidi ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Afrika.

Mchezo wa awali utafanyika kati ya Agosti 18 hadi 20, 2023 ugenini kabla ya mechi ya marudiano kupigwa kati ya Agosti 25 hadi 27, Azam Complex.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo, atakutana na Club Africain ya Tunisia, kwenye raundi ya pili na atakayevuka hapo atatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab