National News

NDEJEMBI AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA UJENZI SHULE YA MSINGI JAJE

Tarehe: 17 Dec, 2023


Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI  Deogratius Ndejembi amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga kuwasimamisha kazi wahandisi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Issa Mchezo na Mussa Mkonachi kutokana na usimamizi mbovu wa miradi huku akiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza manunuzi katika ujenzi wa Shule ya Msingi Jaje.

Ndejembi ametoa agizo hilo jijini Tanga katika ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Jaje iliyojengwa kupitia mradi wa BOOST na Shule ya Sekondari Magaoni iliyojengwa kwa fedha za mradi wa SEQUIP.

“Serikali hii ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haitamvumilia mtumishi yeyote ambaye atashindwa kusimamia miradi kwa uadilifu. Tutachukua hatua kwa watendaji watakaocheza na fedha za miradi ikiwa ni pamoja na kuka na fedha bila kutumika na kuchelewasha ukamilikaji wa miradi. Hivyo mhandisi wa hapa umeonesha udhaifu huo na hivyo nimuagize Mkurugenzi wa Jiji awasimamishe kazi kwa uzembe huo." - Ndejembi

“ TAKUKURU niwatake mlete timu yenu mara moja ya uchunguzi ili mchunguze manunuzi kwenye miradi hii. Haiwezekani Jiji la Tanga saruji iuzwe bei ya juu zaidi ya Pangani. Chunguzeni na ripoti yenu tuipate lakini pia mchukue hatua za kisheria,” amesema Ndejembi.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab