National News

VAR KUANZA KUTUMIKA LIGI KUU TANZANIA BARA

Tarehe: 16 Dec, 2023


Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania Wallace Karia amesema katika juhudi za kukuza soka la Tanzania, (TFF) imepokea mashine za VAR zitakazotumika kuratibu soka Tanzania kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Karia ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa 18 wa TFF mkoani Iringa mbele ya wajumbe wa mkutano huo.

Karia amesema hayo ni mafanikio makubwa kwa Tanzania kwani zitasaidia kuleta ufanisi wa uamuzi wa matokeo wakati wa michezo na kuondoa malalamiko ambayo hujitokeza mara kwa mara.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania