National News

WALIOPOTEZA VYETI HANANG KUPEWA VYETI MBADALA

Tarehe: 16 Dec, 2023


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Said Ally Mohamed amesema kutokana na janga lililowakumba wananchi wa Hanang katika mkoa wa Manyara anatambua wapo waliopoteza vyeti vyao, hivyo wanatarajia kuwapatia vyeti vya mbadala.

Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya NECTA mkoani Dar es Salaam,  Dkt. Mohamed ametoa pole kwa waathirika wote wa maporomoko hayo na amesema kutokana na majanga hayo, NECTA imekuwa ikitoa mchango kupitia taasisi za umma na pia itatoa vyeti mbadala kwa wote waliopoteza vyeti vyao kwenye maafa ya Hanang.

"Wale waathirika wote waliopotelewa na vyeti, baraza litawapatia vyeti mbadala," amesema Dkt. Mohamed.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania






  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab