National News

NIDA NA RITA ZAUNGANISHWA KUWA TAASISI MOJA

Tarehe: 15 Dec, 2023


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo leo Desemba 15, 2023 imetangaza kufuta mashirika manne na kuunganisha mashirika na taasisi za umma 16. 

Akizungumza leo Prof. Mkumbo amesema Mashirika yaliyounganishwa ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na yanaunganishwa na kuunda taasisi moja inatayohusika na utambuzi wa matukio muhimu maishani na lengo ni kutekeleza maelekezo ya Rais Samia  ya kuwa namba moja ya utambulisho (Single Identification Number).

Mashirika mengine yaliyounganishwa ni Bodi ya Chai inaunganishwa na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima wadogo wa Chai Tanzania zinaunganishwa ili kuwa na bodi moja (Bodi ya Chai).

Bodi ya Nyama inaunganishwa na Bodi ya Maziwa zinaunganishwa ili kuunda Taasisi moja ya kuendeleza na kusimamia mazao ya mifugo yakiwemo ya nyama na maziwa.

Kituo cha zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini, Taasisi ya Uhandisi na Usanifu mitambo Tanzania (TEMDO) na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO) zinaunganishwa ili kuunda Taasisi moja.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania