National News

ANDENGENYE ATOA WITO WANANCHI NA WADAU KUTOA USHIRIKIANO KATIKA UKUSANYAJI TAKWIMU KIGOMA

Tarehe: 14 Dec, 2023


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ametoa wito kwa kaya na taasisi zilizochaguliwa kwa ajili ya tafiti za kitakwimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii kwa mwaka 2023/24 pamoja na kilimo wa mwaka 2022/2023 na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa wadadisi wanaoendelea na kazi hiyo ndani ya mkoa wa Kigoma ili tafiti hizo ziweze kuleta matokeo bora kulingana na hali halisi iliyopo

Andengenye ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kubainisha kuwa takwimu zitakazopatikana katika zoezi hilo zitasaidia kutumika na serikali katika kutunga na kuhuisha sera na kupanga mipango pamoja na program za maendeleo katika ngazi ya taifa, kikanda na kimataifa na kubainisha kuwa Ofisi ya  Taifa ya  Takwimu inawahakikishia wadau wote kuwa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu sura 351 taarifa zote zitakazokusanywa zitakuwa siri ambapo zitatumika kwa madhumuni ya kitakwimu.

Kwa upande wake Meneja wa Takwimu Mkoa Suma Robert Tebela amesema kuwa zoezi hilo linafanyika katika Halmashauri zote za mkoa wa Kigoma na kuongeza kuwa kwa upande wa utafiti wa kilimo utahusisha maeneo 25 ambapo hadi sasa unaendelea na kuwa utafiti huo ni muhimu kutokana na kwamba utasaidia kutoa kanzidata kwa ajili ya tafiti zijazo
 
Aidha utafiti huo unaendelea katika mikoa yote 26 ya Tanzania bara kwa kwa kipindi cha siku 60 kuanzia tarehe 6 Novemba mwaka huu ambapo miongoni mwa taarifa zinazokusaywa ni pamoja na jina la shughuli, eneo au mahali ilipo,anuani ya posta, nambari ya simu, shughuli kuu, hali ya umiliki, mwaka wa shughuli au ofisi kuanza kufanya kazi, mwezi na mwaka wa kufanya shughuli au Ofisi, idadi ya wafanaykazi kwa jinsi na jumla ya mapato kwa mwaka.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania

  • © Copyright - 2024
  • All rights reserved by - MainFm
  • Developed by - Mainfintech Lab