National News

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI KATIKA BODI TATU

Tarehe: 14 Dec, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewateua wenyeviti na makamu wenyeviti wa bodi tatu nchini.

Rais Samia amemteua Jaji Mshibe Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Dokta Emmanuel Mpeta kuwa Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo.

Rais Samia pia amemteua Balozi Adadi Rajabu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Fatma Mohamed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo.

Aidha amemteua Theobald Sabi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania.
..........................
Tufuatilie zaidi kupitia
www.mainfm.co.tz
#instagram @mainfmtanzania
#facebook @mainfmtanzania
#twitter @mainfmtanzania